BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar

BONDIA Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' usiku wa kuamkia leo amempiga kwa TKO raundi ya tatu mpinzani wake Mada Maugo katika pambano la ubingwa wa Afrika (Light heavy weight) kwenye uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa PST alisema Maugo amekubali matokeo licha ya kutaka mechi ya marudiano hata isipokuwa ya ubingwa ili tu alipe kisasi huku akikiri kukoshwa na viwango vilivyooneshwa na mabondia wote waliopanda ulingoni.

"Kiukweli mabondia walijitahidi kucheza vizuri na kuwavutia waliohudhuria na kufanya kushangiliwa na mashabiki kwa muda wote wa mchezo." alisema Luta.

Aidha katibu huyo alisema hakupata malalamiko yoyote kutoka kwa mabondia kuhusu malipo yao kwavile kila kitu kiliwekwa sawa na promota wa pambano hilo Kaike Siraju.

Kwa upande wake promota huyo alisema amejipanga kuandaa mapambano mengi ndani ya mwaka huu na kujumuisha mabondia kutoka nje ya nchi ili kuinua mchezo wa masumbwi nchini.

Katika mapambano mengine bondia Mohamedi Matumla alitoka sare na Cosmas Cheka huku Nasib Radhamani akitoka sare na Fransis Miyeyusho ingawa mashabiki wa mabondia hao walishindwa kukubali matokeo kwa kuamini kuwa  bondia wao alishinda . Pia kulitokea vurugu za hapa na pale lakini hakuna aliyepata madhara.

Post a Comment

 
Top