BOIPLUS SPORTS BLOG

BEKI wa kulia wa klabu ya Sunderland Emmanuel Eboue amefungiwa mwaka mmoja kutojihusisha na masuala ya soka baada ya kushindwa kumlipa wakala wake Sebastien Boisseau.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 alitakiwa na kamati ya hadhi ya wachezaji ya FIFA kumlipa wakala wale huyo lakini yeye alikataa rufaa ya maamuzi hayo  kwenye mahakama ya usuluhishi ya michezo (CAS) na rufaa hiyo kutupwa kapuni.

Eboue raia wa Ivory Coast ambaye amejiunga na Sunderland anatakiwa kutumikia kifungo chake cha mwaka mmoja nje ya soka au amlipe deni lake lote wakala huyo .

Kwa upande wake klabu ya Sunderland imepanga kuvunja mkataba na beki huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal na Galatasaray endapo atashindwa kulipa deni hilo.

Post a Comment

 
Top