BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar
KIUNGO wa Azam Fc na timu ya taifa ya Tanzania  'Taifa Stars', Himid Mao leo amepata ajali akiwa anaendesha gari yake aina ya Nissan Xtrail maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Himid ambaye aliichezea timu yake jana ilipopambana na Yanga na kutoka sare aliiambia BOIPLUS kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa sita mchana akiwa anatoka katika eneo la kuegesha magari ndipo gari nyingine aina ya Toyota Noah ambayo ilikuwa kasi ilipotokea ghafla na kumgonga.

"Sijaumia, ila gari ndio imeharibika. Nilikuwa natoka hapa Parking Mlimani City ndio jamaa akaja spidi na kunivaa." alisema Himid

Post a Comment

 
Top