BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi 'Mido'
 Straika wa Yanga, Amissi Tambwe kushoto akisaka mbinu za kuwatoka walinzi wa Azam FC huku Juma Abdul akiwa tayari kutoa msaada


 Thaban Kamusoko na Vicent Bossou wakimchunga Kipre Tchetche wa Azam asilete madhara langoni mwao


 Marafiki wa zamani wakakutana, Tambwe na Ramadhan Singano 'Messi' ambao walicheza Simba katika kipindi kimoja kwa mafanikio makubwa, jana walikutana wakiwa na 'dini' tofauti


 Beki anayeongoza kwa idadi ya mabao kwenye ligi kuu ya Vodacom, Shomari Kapombe  akijiandaa kumzuia Mwinyi Haji wa Yanga. Beki huyo anazidiwa na washambuliaji tu kwa idadi ya mabao huku yeye akiwa amefunga saba


 Vita ya Pascal Serge Wawa na Donald Dombo Ngoma haikuwa ya 'kitoto'


 Wachezaji wa Yanga Deus Kaseke, Simon Msuva, Kelvin Yondan (5) wakimpongeza Juma Abdul (anayetazamana na Yondan) baada ya kuisawazishia timu hiyo


 Wachezaji wa Azam wakipongezana baada ya Juma Abdul wa Yanga kujifunga bao la kwanza


 Beki wa Azam Said Morad akipambana na Ngoma


 Juma Abdul akishangilia bao lake la kusawazisha


 Mashabiki wa Azam na Yanga waliokaa katika jukwaa la Mashariki wakishambuliana kwa kurushiana viti wakati mchezo ukiendelea

 'Peace and Love'......Tchetche, Kamusoko na Abdul, Morad wakipongezana baada ya mechi


 Kikosi cha Azam kilichoanza jana dhidi ya Yanga


Kikosi cha Yanga kilichoanza jana dhidi ya Azam Fc

Post a Comment

 
Top