BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar


KWENYE mitandao ya kijamii jana ilisambaa picha inayowaonyesha kocha wa Yanga Hans Pluijm na wa APR Nizar Khanfir wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo wa leo unaowakutanisha vigogo hao wa Afrika Mashariki.

Kilichowastaajabisha watu katika picha hiyo ni kushindwa kwao kuelewa hii mechi ni ya Ligi kuu ya Vodacom, ya Timu ya Taifa au klabu bingwa Afrika?. Na hiyo ilitokana na bango lililowekwa nyuma ya makocha hao kuwa na matangazo ya NHIF, Vodacom, Azam Tv, Star Tv, Startimes na Airtel wakati hao si wadhamini wa Yanga ambayo ndiyo yenye mchezo huu wa leo.


BOIPLUS iliandika makala na ndani yake ikalizungumzia jambo hili kuwa bango hilo lilipaswa kuwa na tangazo la mdhamini wa Yanga pekee ambaye ni Kilimajaro na si vinginevyo.

Kwa kuliona hilo, wahusika wa maandalizi ya mechi hii wamechukua hatua na leo katika ukumbi ambao utafanyika mkutano wa makocha na waandishi wa habari pamepambwa kwa mabango yanayoonyesha nembo ya Yanga na Kilimanjaro pekee. 

BOIPLUS inawapongeza kwa marekebisho hayo na hii ndio maana halisi ya kuchukulia maoni ya watu wengine katika njia chanya.

Post a Comment

 
Top