BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Rusumo


MTU kwao jamani.......mara baada ya kuvuka mpaka wa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, wafanyabiashara kadhaa waliosafiri na mashabiki kwenda Kigali walijaribu kufungua maduka ya muda ya kuuza jezi. Lakini unajua kilichotokea?, kila mtu alikuwa akiulizia jezi ya Haruna Niyonzima.

Wafanyabiashara hao ambao husafiri na timu mikoani na hata nje ya nchi walipoona neema hiyo wakaamua kupandisha bei na kuziuza kwa Sh 15,000 hadi 20,000 badala ya Sh 10,000 ambayo ndio bei ya kawaida ya jezi hizo za kiwango cha kati.

Kupandishwa kwa bei hiyo hakikuwa kikwazo kwa mashabiki hao ambao waliendelea kuzigombea kama vile zinauzwa kwa bei ya pipi na hadi basi la mashabiki hao linaondoka wafanyabiashara hao walikuwa 'njema' huku wakiondoka na matumaini kibao kuwa zilizobaki zitaenda kumalizikia jijini Kigali ila wakihofia taratibu za huko kama zitawaruhusu kuzimwaga mtaani.

"Kila mtu anataka jezi ya Niyonzima. Mauzo tuliyofanya hapa yanatupa matumaini ya kwenda kuuza sana Kigali ingawa hatujui huko taratibu zao zikoje, wakituzuia kuzimwaga mtaani itakula kwetu." alisema mmoja wa wafanyabiashara hao anayejulika kwa jina maarufu la Jecco.


Post a Comment

 
Top