BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
Mfungaji wa bao pekee la Kagera Sugar, Mbaraka Yusuf

TIMU ya soka ya Kagera Sugar leo imefanikiwa kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa nyavuni katika dakika ya 12 mfungaji akiwa ni Mbaraka Yusuf. Baada ya hapo timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hadi dakika 45 za kwanza zinakamilika hakukuwa na bao lingine.

Kipindi cha pili timu hizo za watengeneza sukari ziliendelea kutengeneza mashambulizi kadhaa ingawa mipango mingi iliishia njiani huku zikionekana kutozidiana sana viwango na hadi mwisho wa mchezo wenyeji Kagera ndio waliondoka na pointi tatu.

Kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime alisema amekubali matokeo na wanajipanga kwa mchezo unaofuata kwavile mpira wa Tanzania uko hivyo hivyo siku zote kwahiyo hata akisema zaidi ataonekana mlalamishi tu. Kwa upande wa kocha Kagera Adolf Rishard yeye amefurahishwa na matokeo kwavile wamekuwa hawafanyi vizuri siku za hivi karibuni.

Kwa matokeo hayo Kagera imepanda hadi nafasi ya 11 kwa kufikisha pointi 25 huku Mtibwa wakibaki kwenye nafasi ya nne kwa pointi zao 39

Post a Comment

 
Top