BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MSHAMBULIAJI wa Simba, Raphael Kiongera jana alijiunga na kambi ya timu hiyo iliyowekwa mkoani Morogoro huku akianza mazoezi mepesi ambapo anatumia saa moja tu na kupumzika wakati wenzake wakiendelea na mazoezi hayo.

Simba inajiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo City wao wanatarajia kutua jijini muda wowote.

Kiongera ambaye alikuwa nje ya kikosi kwa zaidi ya wiki tatu akisumbuliwa na nyonga ameanza mazoezi hayo mepesi ingawa mechi ijayo hataweza kucheza kwani hatakuwa fiti kwa ajili ya pambano hilo lenye upinzani mkubwa.

"Naendelea vizuri na nipo Morogoro sasa, nafanya mazoezi mepesi mpaka hapo baadaye ambapo nitaruhusiwa kufanya mazoezi ya ushindani, kwasasa natumia saa moja tu kufanya mazoezi yangu pembeni ya uwanja," alisema Kiongera.

Post a Comment

 
Top