BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, DarTIKETI za mchezo wa marudiano raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC na APR ya Rwanda zitaanza kuuzwa siku ya mchezo, jumamosi huku kiingilio cha chini katika mchezo huo kikitajwa kuwa ni Sh. 5,000. Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Habari na

Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro ameiambia BOIPLUS kwa  njia  ya simu  kwamba kiingilio hicho kitakuwa ni kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.

"Kwa ujumla eneo lote la mzunguko linalohusisha viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu watu wataketi kwa Sh. 5,000 huku VIP A tiketi yake itanunuliwa kwa Sh. 25,000, VIP B na C kote kila tiketi itauzwa kwa Sh.20,000.


"Tiketi zitaanza kuuzwa mapema siku ya mchezo katika maeneo ya siku zote, ikiwemo  Uwanja wa Karume na Uwanja wa Taifa." alisema Muro.


 Yanga itaingia katika mchezo wa Jumamosi ikiwa na nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Amahoro jijini Kigali.

Post a Comment

 
Top