BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar

Nahodha Mbwana Samatta akiwaongoza wenzake kupasha misuli kabla ya kuanza kusikiliza 'maufundi' ya kocha Boniface Mkwasa

'No pain no gain'......Thomas Ulimwengu akipata huduma ya kwanza baada ya kupata maumivu mazoezini


Samatta ndiye aliipatia Stars bao pekee ilipopambana na Chad katika mchezo wa awali, je atafanya hivyo tena hapo jumatatu?


Samatta akikwepa vikwazo ili kujiweka fiti katika kupambana na walinzi wa Chad


Mlinzi wa kushoto wa Stars Mohamed Hussein 'Tshabalala' akifanya kazi ili kumshawishi Mkwasa ampange dhidi ya Chad


Himid Mao amekuwa msaada mkubwa katika eneo la kiungo akishirikiana vema na Jonas Mkude


Mshambuliaji wa Mansfield ya Uingereza, Adi Yusuf akitafuta mbinu za kumtoka Tshabalala


Beki wa kushoto Haji Mwinyi akipiga krosi . Mlinzi huyu amekuwa bora zaidi kwenye kupiga krosi na pasi za mwisho


Kipa Aishi Manula akiokoa penati ya Ally Mustafa 'Barthez' katika mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa taifa jana


John Bocco 'Adebayor' anapambana kuingia kwenye kikosi cha kwanza huku akikutana na changamoto kutoka kwa mastraika wengine kama Elius Maguri na Adi


Mkwasa akitoa maelekezo kwa washambuliaji wake


Manula ametokea kuaminika zaidi na makocha wa Stars, je atapewa jukumu hilo jumatatu

Bwana mdogo Farid Mussa katikati akikatiza katikati ya mabeki Mwinyi (kushoto) na Juma Abdul. Farid alitoa pasi ya bao lililofungwa na Samatta

Kipa Shaban Kado akipokea maelekezo toka kwa mkongwe Peter Manyika

Barthez ni mzoefu, uwepo wake katika kikosi ni faida nyingine kwa Stars ambayo haipaswi kupoteza alama

Shomari Kapombe, beki anayeongoza kwa mabao kwenye ligi kuu ya Vodacom, amekuwa mtu muhimu kwenye kuanzisha mashambulizi


Post a Comment

 
Top