BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
USIKU huu kulikuwa na mechi kadhaa za kusisimua barani Ulaya ambapo vigogo kadhaa vilikuwa uwanjani vikisaka pointi tatu muhimu katika michezo ya ligi kuu.

Nchini Uingereza Arsenal ikiwa nyumbani ikalala mabao 2-1 dhidi ya Swansea City. Mabao ya Swansea yakifungwa na Wyne Routledge na Ashley Williams katika dakika za 15 na 74 wakati lile la Arsenal la kufutia machozi likifungwa na Joel Campbell kwenye dakika ya 32.

Liverpool ikiwa nyumbani ikautumia vema uwanja wao wa Anfield baada ya kuibugiza Manchester City mabao 3-0. Adam Lallana, James Milner na Roberto Firmino wakipeleka kilio kwa matajiri wa jiji la Manchester katika dakika za 34, 41 na 57.

Manchester United wao waliondoka na pointi tatu dhidi ya Watford. Shukrani kwa bao la 'jioni' la Juan Mata alilotupia katika dakika 83.

Nchini Hispania, Real Madrid wakiwa ugenini wameifunga Levante mabao 3-1. Christiano Ronaldo akifunga bao la kwanza kwa penati katika dakika ya 34 kabla kipa wa Levante, Diego Marino hajamalizia wavuni shuti la kinda Mayoral na kuipa Madrid bao la pili.

Dakika ya 39, Deyverson aliipatia bao safi Levante. Isco aliyeingia badala ya James Rodriguez aliifungia Madrid bao la tatu kwenye dakika ya 90 akimalizia pasi safi ya Ronaldo.

Video za mabao yote zinapatikana kwenye ukurasa wetu wa Instagram @boiplus_blogspot

Post a Comment

 
Top