BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MARA kadhaa kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya wachezaji nyota wa Stand United kutotendewa haki na kocha wao Mfaransa Patrick Liewig, miongoni mwao ni Elius Maguri.

Hivi karibuni Maguri amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kama ilivyokuwa hapo awali sababu kubwa ni kocha huyo kusisitiza kuwa wachezaji wake nyota wana utovu wa nidhamu.

Hata hivyo, Maguri ambaye ana mabao 10 mpaka sasa amesisitiza kuwa amejifunza uvumilivu kwenye kikosi cha Liewig pamoja na changamoto zote anazozipata kwani anajuwa malengo yake kwenye soka ni yapi.

''Mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu na nitaamua niende wapi kwa ajili ya msimu ujao, kupitia Stand nimejifunza mengi kubwa ni uvumilivu kwani najua ni kitu gani nahitaji kwani mchezaji hupaswi kukata tamaa na ukifanya hivyo huwezi kufanikiwa.

''Nina michakato yangu ninayofanya ambayo kwasasa siwezi kuiweka hadharani kwani bado haijakamilika ila naamini hapo baadaye kila kitu kitakuwa wazi,'' alisema Maguli

Hata hivyo kuna taarifa kwamba timu ya Al Ahly ya Misri ni miongoni mwa timu zinazomuwania ikiwemo Yanga ya jijini Dar es Salaam ingawa yeye amekiri kuwepo kwa mpango huo na Al Ahly huku upande wa Yanga akisisitiza kuwa hafahamu lolote na kama watamuhitaji hatasita kufanya nao mazungumzo.

Post a Comment

 
Top