BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Kariim Boimanda


MASHABIKI wa soka jijini Kigali wameonyesha kusikitishwa sana na kitendo cha mechi ya Yanga dhidi ya APR  iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa kutoonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni  kama ambavyo walitarajia.

Mashabiki kadhaa nchini Rwanda walianza kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenye namba ya simu ya BOIPLUS huku wengine wakituma barua pepe za kuulizia ni kituo gani cha televisheni kitarusha mchezo huo. Walipojibiwa kuwa mechi hiyo isingerushwa moja kwa moja wengi walionyesha kusikitika huku wakihoji kwanini isirushwe.

"Hao Yanga kwanini wakatae mechi isirushwe, wana matatizo gani?. Hawajua wana mashabiki wengi huku, hata Rais Kagame (Paul) ni shabiki mkubwa wa soka hatofurahi kusikia mechi haionyeshwi." alilalama mmoja wa mashabiki wa soka wa jijini Kigali.Mwandishi wa habari za michezo jijini Kigali aliyefahamika kwa jina moja la Kazungu alisema huko kwao wanaichukulia Tanzania kama nchi iliyopiga hatua kubwa kwenye soka hivyo hawakutarajia kuona mechi kubwa kama hiyo inashindwa kuonyeshwa.

"Watu wanalalamika sana kukosa kuitazama mechi hiyo, kama tatizo ni mapato ya mlangoni basi wangeruhusu hata televisheni ya Taifa ionyeshe kwa kushtukiza kama ambavyo RBA ilionyesha mechi ya huku. " alisema Kazungu.

Taarifa ambazo zilienea mitaani jana ni kwamba klabu ya Yanga ilishindwa kuafikiana na Azam Tv juu ya taratibu za kurusha pambano hilo, Yanga wakitaka mechi isitangazwe kabla kuwa itaonyeshwa 'live' jambo ambalo watu wa Azam Tv hawakuliafiki. 

Post a Comment

 
Top