BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
Mussa Mgosi akiwa ameketi kwenye viti vinavyokaliwa na viongozi wa benchi la ufundi.

KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amempa majukumu mapya nahodha wake Musa Mgosi ambapo sasa anamtumia kama kocha mchezaji wa kikosi hicho.

Hivi karibuni Mgosi ameonekana akishirikiana vyema na Mayanja katika kumpa maelekezo kadhaa kwenye mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara.

Mgosi ameiambia BOIPLUS kuwa kocha wake alimuomba awe anamsaidia katika kumwongoza kwenye baadhi ya mambo ikiwemo mazoezi na hata uwanjani hasa pale inapobidi

"Kocha mwenyewe aliniomba kumsaidia baadhi ya mambo hivyo aliniongeza majukumu tu. Ni nahodha na sasa ni kocha mchezaji na ndiyo maana mara kadhaa kwenye mechi huwa nakaa karibu naye," alisema Mgosi

Akielezea mbio zao za ubingwa, Mgosi alisema "Naamini tutatwaa ubingwa kwani tuna nafasi hiyo na tunaendelea kupigania ili tufanikishe hilo, kikubwa ni kuongeza juhudu na kumuomba Mungu,"

Post a Comment

 
Top