BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda


MENEJA wa timu ya KRC Genk anayochezea mtanzania Mbwana Samatta, Tony Greco amefariki dunia alfajiri ya leo kwa ugonjwa wa kansa huko Genk Ubelgiji.

Tony ambaye imeelezwa kuwa kansa iliuathiri mwili wake wote aliondoka klabuni hapo kama wiki tatu zilizopita ili kwenda kupata matibabu hospitalini hadi alipoiaga dunia leo.Akizungumza na BOIPLUS, Samatta ambaye alipokelewa na meneja huyo alipotua Genk alisema wachezaji na wafanyakazi wa timu hiyo wameshtushwa sana na kifo cha Tony na kwamba amewaachia pengo kubwa .


"Tumeumizwa sana kwavile kama unavyojua meneja ndio mtu yupo karibu zaidi na wachezaji." alisema Samatta

Post a Comment

 
Top