BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi wetu, Kigali

Straika wa Amavubi, Sugira Ernest akishangilia moja ya mabao yake mawili dhidi ya Mauritius leo

TIMU ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' leo imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuirarua Mauritius kwa mabao 5-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa jijini Kigali.

Katika mchezo wa awali ambao ulichezwa nchini Mauritius, wenyeji waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kiwafanya vijana hao wa Paul Kagame warejee nchini Rwamda kinyonge wakiwa na dege lao walilopewa na Rais huyo mpenda michezo.

Mabao ya Amavubi leo yalipachikwa wavuni na Nshuti Savio wa Rayon Sports katika dakika ya 11 kabla Sugira Ernest anayeichezea AS Kigali hajapachika mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 30 na 31.

Kipindi cha pili karamu ya mabao iliendelea ambapo katika dakika ya 71, mlinzi wa Kiyovu  Ombolenga Fitina aliipatia Amavubi bao la nne huku kiungo wa Azam FC ya Tanzania, Jean Claude Mugiraneza 'Migi' akifunga kitabu cha mabao ya leo kwa bao safi la dakika ya 89.

Kwa ushindi huo Amavubi imesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1.

Post a Comment

 
Top