BOIPLUS SPORTS BLOG

Cairo, Misri


TIMU ya Taifa ya Misri jana imeibutua Nigeria bao 1-0 katika mchezo wa kundi G wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON), uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Cairo.

Mchezo huo ulikuwa ni mkali na wa kusisimua hasa pale ilipoonekana kila timu ikipambana kupata ushindi utakaoiongezea matumaini ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazopigwa mwakani nchini Gabon.

Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa nyavuni na Ramadhan Sophy katika dakika 65 baada ya shuti lake kuguswa na beki wa Nigeria ambaye alimfanya kipa wake kupotea 'maboya'.

Kwa ushindi huo Misri inakuwa imejikusanyia pointi 7 ambazo zinaweza kufikiwa na Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' pekee kama itashinda mechi zake mbili zilizosalia, Nigeria yenye pointi mbili imeshaondolewa kwenye mbio hizo kwavile hata ikiifunga Stars katika mchezo wake wa mwisho, itafikisha pointi tano tu.

Ili Stars ifuzu ni lazima iifunge Misri mabao 4-0 na kuendelea halafu ikapate ushindi wowote dhidi ya Nigeria.

Post a Comment

 
Top