BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar

KLABU ya Ndanda FC 'Wana Kuchele' ya mkoani Mtwara wamejinasibu kuwatoa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu Yanga kwenye mchezo wa robo fainali wa kombe la FA utakaochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kesho.

Akizungumza na BOIPLUS Msemaji wa klabu hiyo Idrisa Bandari alisema kuwa wamejipanga kufanya maajabu kwenye mchezo wa kesho na hawaiogopi Yanga, watapambana kuhakikisha wanatinga nusu fainali ya michuano hiyo.

"Itakuwa mechi ngumu kwetu na kwao pia lakini wachezaji wetu wameandaliwa kwa muda wa wiki moja na wapo vizuri kuhakikisha wanaitoa Yanga hapo kesho," alisema Bandari.

Aidha Afisa habari huyo alisema kocha wa muda wa timu hiyo Abdul Mingange ataendelea kuwa na timu huku kocha mkuu Malale Hamsini akitarajiwa kujiunga na hivi karibuni.

Ndanda wataongozwa na ushambuliaji wake hatari Atupele Green huku pia wakiwategemea wachezaji wenye uzoefu kama Wiliam Lucian 'Gallas', Paul Ngalema na nahodha Kiggi Makasi ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga miaka nyuma.

Timu hiyo ambayo imekuwa ikipambana dakika zote 90 za mchezo imekuwa ikipewa nafasi ndogo ya kushinda mchezo huo japokuwa katika mpira kila kitu kinawezekana.

Post a Comment

 
Top