BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally na Marco Ngavenga, Mbeya

PRISONS leo imelipa kisasi kwa kuifunga Stand United bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Prisons ilipata bao hilo dakika ya 19 ya mchezo likifungwa na Lambert Sibianka aliyepiga shuti kali na safi akiwa ya nje 18 baada ya kuupata mpira uliokuwa ni wa piga nikupige langoni mwa wapinzani wao.

Bao hilo lilidumu mpaka mwisho mwa mchezo huku Kocha wa Stand United, Patrick Liewig alilikubali bao hilo kwamba ni bao safi ambapo wachezaji wake walipata nafasi ila walishindwa kuzitumia.


Kwa matokeo hayo Prisons imefikisha pointi 35 huku Stand United ikibaki na pointi zile zile na wanaisubiri Mbeya City katika mechi yao ya Jumatano itakayochezwa Uwanja wa Sokoine.

Stand ambayo ilijiamini kushinda mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kuilaza Prisons mechi ya awali kwa bao 3-0 inahitaji ushindi wa hali na mali ili angalau kuondoka na pointi tatu za ugenini.

Post a Comment

 
Top