BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda


STRAIKA wa KRC Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amefunguka kuwa anafurahi kuona kila siku mambo yake yanazidi kuwa mazuri katika klabu yake mpya ambayo amejiunganayo mwezi januari akitokea TP Mazembe ya DR Congo.

Samatta aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya nchini Ubelgiji kati ya Genk na KV Oostende na wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 huku Samatta akitupia bao moja ambalo lilikuwa la kwanza katika mchezo.

"Mambo yanaenda poa kaka, nafurahi sana kuona kila siku kuna mabadiliko chanya. Kwangu hii ni changamoto na inanifanya nizidi kukomaa zaidi." alisema Samatta ambaye ana mabao mawili tangu ajiunge na wabelgiji hao.

Hii ni mara ya kwanza kwa Samatta kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Mechi zilizotangulia alikuwa akiingia badala ya straika wa kutumainiwa wa timu hiyo, mgiriki Nikos Karelis ambaye jana alianzia benchi.

Samatta ambaye ni nahodha mpya wa Taifa Stars atajiunga na timu hiyo nchini Chad akitokea Ubelgiji. 

Post a Comment

 
Top