BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainab Rajabu, DarSIMBA imerudi kileleni kwa kuifunga Ndanda FC mabao 3-0 hivyo kurudi kwenye nafasi yake ambayo ilishushwa na watani wao Yanga. Mechi hiyo ikichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Hamisi Kiiza akifikisha mabao 18 baada ya leo kupiga bao mbili kati ya hizo.

Matokeo hayo yameifanya Simba ifikishe pointi 51 huku Yanga ikiwa na pointi 50 na mechi moja mkononi wakati Azam wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 47 na mechi mbili za vipara mkononi.

Simba ilianza kupata bao lake la kwanza dakika ya 36 kupitia kwa kiungo wao Mwinyi Kazimoto akipokea pasi safi iliyopigwa na Hassan Kessy huku Kiiza akiifungia mabao dakika ya 57 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajibu huku bao la tatu likifungwa dakika ya 73 akipokea pasi ya Danny Lyanga.
Makocha wa timu zote mbili wa Simba na Ndanda walifanya mabadiliko ya vikosi vyao ambapo Jackson Mayanja aliwatoa Said Ndemla, Ajibu, Kazimoto nafasi zao zilichukuliwa na Awadh Juma, Danny Lyanga pamoja na Musa Mgosi.

Kocha wa Ndanda Fc, Hamisi Malale yeye aliwatoa Omega Sema, Omar Mponda na Kigi Makasy ambapo nafasi zao zilichukuliwa na Bryson Raphael, Salum Mineli na Ahmad Msumi.

Timu zote zilicheza kwa kushambuliana lakini Ndanda walishindwa kuwa na mbinu za kutikisa nyavu za wapinzani wao kila walipokuwa wanafika golini kwa Simba huku mwamuzi wa mchezo huo Jimmy Fanuel kutoka Shinyanga  akitoa kadi ya njano kwa Salvatory Ntebe wa Ndanda baada ya kumchezea rafu Ajibu

Post a Comment

 
Top