BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi WetuKLABU ya Simba imepokea kwa mshituko taarifa ya kipa wao wa zamani Abel Dhaira ambae amepata na ugonjwa wa kansa ya tumbo.

Dhaira ambaye aliwahi pia kuwa golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda na anayechezea klabu ya IBV Vestmannaeyiar ya Iceland alipata kuichezea Klabu ya Simba kwa mafanikio makubwa miaka michache iliopita.Klabu imepokea taarifa za ugonjwa huo kwa taharuki kubwa na inaungana na Dhaira pamoja na familia yake kwenye kipindi hiki kigumu cha maradhi hayo makubwa

"Tunaamini licha ya matibabu atakayoyapata kipa huyo pia nguvu ya Mwenyezi Mungu inahitajika katika kumponyesha nyota wetu huyo," alisema Haji Manara katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Alhamis.


Taarifa za ugonjwa wa Dhaira zilianza kusambaa juzi kwenye mitandao mbalimbali ya jamii ambapo mpaka sasa yupo hospitali akiendelea na matibabu.

Post a Comment

 
Top