BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Marco Ngavenga, Mbeya


MBEYA City leo imetumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kuvuna pointi tatu dhidi ya Stand United kwa kuifunga bao 2-0. Mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Hii ni mechi ya pili kwa Stand United kupoteza kwenye Uwanja huo baada ya mechi ya awali kufungwa na Prisons bao 1-0 na sasa wataelekea Songea kucheza na Majimaji huku Mbeya City itakuwa ugenini kucheza na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


Mbeya Citu ilianza kupata bao lao la kwanza dakika ya 13 kupitia kwa mshambuliaji wao Rafael Alpha aliyepiga penati iliyopanguliwa na kipa wa Stand, Frank Muwonge na kurudi ndani ambapo Rafael aliupata na kufunga.Penalti hiyo ni baada ya beki wa Stand, Abssouman Guessan kuugusa mpira kwa mkono mpira ambao ulikuwa wa faulo iliyopigwa na Ramadhan Chombo 'Redondo'.

Dakika ya 47, Haruna Shamte aliipatia Mbeya City bao la pili alilolifunga kwa mpira wa adhabu ndogo nje ya 18. Faulo hiyo ilitokea baada ya  Redondo kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Stand United.

Kwa matokeo hayo Mbeya City inayofundishwa na Mmalawi, Kinnah Phiri imefikisha pointi 24 ikipanda mpaka nafasi ya tisa huku Stand wakibaki na pointi zao 30 na wanashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.

Post a Comment

 
Top