BOIPLUS SPORTS BLOG

AZAM Fc imepaa leo kwenda nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wa kwanza kombe la Shirikisho dhidi ya Bidvest Wits


Azam imeondoka na wachezaji wake nyota wote huku wakiwa na matumaini tele ya kwenda kupata matokeo mazuri yatakayowarahisishia kupata nafasi ya kusonga mbele baada ya mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam


Azam inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ya Vodacom wakiwa na pointi 47 na mchezo mmoja mkononi. Yanga inaongoza kwa pointi 50 huku Simba ikiwa ya pili kwa pointi 48

Azam na Yanga zinaiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ambapo Yanga wanaoshiriki ligi ya mabingwa Africa wataifuata APR ya Rwanda kesho

Post a Comment

 
Top