BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar
YANGA inaondoka leo kwa ndege kwenda Kigali kuvaana na APR siku ya jumamosi katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika. Lakini asubuhi ya leo mashabiki takribani 35 wameondoka kwa basi la kukodi kwenda kuipa sapoti timu yao.

Hizi hapa ni picha za matukio yaliyojiri katika makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga na Jangwani wakiwa wanaianza safari yao.

 Mzee Akilimali ambaye ni mkuu wa msafara akiwa amepozi kuanza safari


 Hapa mashabiki hao waliamua kufunga bendera ya Taifa mbele ya basi lao ili kuonyesha utaifa


 Mashabiki wakisubiri utaratibu wa kuingia kwenye basi ili kuanza safari


 Muonekano wa makao makuu ya Klabu ya Yanga alfajiri ya leo


 Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro alipita klabuni hapo kuhakikisha kila kitu kimekaa sawa kwa ajili ya mashabiki hao kuanza safari


Mzee Akilimali akitoa maelekezo ya safari kwa shabiki aliyefahamika kwa jina la Sinzo


 Mmoja wa waratibu wa safari hiyo, Godlisten 'Chicharito'

 Hili ndilo basi wanalosafirinalo mashabiki wa Yanga kuelekea Kigali
Boiplus Blogspot itakuletea matukio yote yatakayojiri kabla, katika mchezo na baada ya mchezo huo.
Tembele Blogsite yetu pamoja na kurasa za:
Facebook: Boiplus Blogspot
Instagram: @boiplus_blogspot
Twitter: @BoiplusBlogspot

Post a Comment

 
Top