BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda

KLABU ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji imemtumia ujumbe mfupi wa maneno straika wao Mbwana Samatta, kumpongeza kwa ushindi walioupata Taifa Stars dhidi ya Chad na hasa bao lake pekee alilofunga jioni ya leo.

Ujumbe huo uliotumwa na Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo De Conde Dimitri uliandikwa kwa lugha ya kiingereza na kiflamish (lugha inayotumika zaidi Genk na inafanana na Kiholanzi).

Samatta ambaye nchini Ubelgiji anajulikana zaidi kwa jina la Aly, aliiambia BOIPLUS kuwa amefarijika kuona klabu yake inamfuatilia na kumpongeza kwa matokeo waliyoyapata na kwamba hiyo ni faida kwa wachezaji wengine kuonekana.

"Wamenipongeza, nimefurahi sana kuona wananitazama, kwahiyo kwa kunifuatilia mimi wanaweza pia kuona na wachezaji wengine kutoka Tanzania, ni fursa kwa namna nyingine." alisema Samatta.

Samatta ameanza leo kuvaa kitambaa cha unahodha wa Stars na kwa inaonyesha ameanza kwa bahati baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini.

Post a Comment

 
Top