BOIPLUS SPORTS BLOG

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesisitiza kuwa hana mpango wa kujiuzulu pamoja na mashabiki wa timu hiyo kukosa imani ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Arsenal wameshinda mechi moja tu kati ya nne za ligi kuu na kuachwa kwa  pointi 11 na vinara Leicester City, huku wakiwa tayari wameshaaga michuano ya FA Cup katika hatua ya robo fainal dhidi ya Watford na kutolewa katika hatua ya 16 bora kwenye ligi mabingwa barani Ulaya na Barcelona.

Akifanya mahojiano na kituo cha habari cha beIN SPORTS cha Ufaransa alipoulizwa kuhusu hatima yake klabuni hapo Wenger alisema 
"Sina wasiwasi kwa kuwa natimiza majukumu yangu kwa asilimia mia moja na siku zote nafanya kila linalowezekana kutimiza malengo na sina wasiwasi kuhusu watu wanazungumza nini kuhusu Mimi

"Wanachozungumza watu ni hisia na maoni na katika kazi yangu naangalia ni jinsi gani timu inafanya vizuri." alisema Wenga.

Mfaransa huyo pia alisema katika maisha anaamini kuwa ni muhimu kuangalia ulichopangiwa kukifanya na yeye ameteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo ili kuifanya timu ifanye vizuri.

Kauli hii inawakata maini mashabiki wa timu hiyo kote ulimwenguni ambao wanaamini ni muda wa kocha huyo kuachia ngazi kwa washika bunduki wa London.

Post a Comment

 
Top