BOIPLUS SPORTS BLOGMICHEZO saba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuchezwa katikati ya wiki hii, kwa kesho kuchezwa mchezo mmoja, huku michezo mingine sita ikichezwa siku za Jumatano na Alhamisi katika viwanja mbalimbali nchini.

Kesho Jumanne, Yanga watakua wenyeji wa Wana Kimanumanu African Sports, mchezo utakaoanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga wana pointi 47 wakiwa nyuma ya Simba wenye pointi 48 hivyo endapo watashinda mechi hiyo wataishusha Simba kileleni ambao watacheza Alhamisi wakiikaribisha Ndanda FC.

Jumatano keshokutwa, Prisons watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Coastal Union wakicheza na ndugu zao maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mwadui FC watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Toto African katika uwanja wa  Mabatini , Mlandizi mkoa wa Pwani.

Alhamisi Simba watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya timu ya Mbeya City wakiwakaribisha Stand United 'Chama la Wana' mechi itakayochezwa katika uwanja wa Sokoine.

Post a Comment

 
Top