BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda


HATIMAYE kile kilichokuwa kikisubiriwa na wadau soka hususani mashabiki wa Yanga kuwa watakutana na timu gani kwenye raundi ya pili ya klabu bingwa Afrika kati ya R.C.D Libolo au Al Ahly, kimewekwa wazi baada Ahly kuibamiza Libolo mabao 2-0 kwenye mchezo uliopigwa nchini Misri.

Jioni ya leo katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga imetoka sare ya bao 1-1 na APR ya Rwanda hivyo kuiondoa mashindanoni kwa jumla ya mabao 3-2. Katika mchezo wa awali jijini Kigali vijana hao wa Jangwani waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Ahly wenyewe walitoka suluhu na Libolo kwenye mchezo wa kwanza kule Angola hivyo ushindi wa leo umewaondoa waangola hao kwa mabao 2-0 na sasa Yanga itavaana na Waarabu hao ambao ni wabishi hasa wakiwa nyumbani kwao.

Yanga haina historia nzuri linapokuja suala la kuziondoa mashindano timu za kiarabu lakini inaonekana mwaka huu wamepania kufika mbali kutokana na usajili kabambe walioufanya.

Post a Comment

 
Top