BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi wetu
MSHAMBULIAJI hatari wa Manchester City, Sergio Aguero ameifungia timu yake magoli matatu peke yake 'hattrick' dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford bridge na kuisaidia kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikionekana kutafuta goli la mapema huku wachezaji Kelvin de Bruyne na Samir Nasri wakiwa ni mwiba mkali kwa vijana hao wa darajani.

Aguero alipata magoli dakika ya 33,54 na 81 huku lile la tatu akilifungwa kwa mkwaju wa penati baada ya golikipa Thibat Cuortious kumchezea rafu Fernandinho na mwamuzi Michael Dean kumuonesha kadi nyekundu ya moja kwa moja.

City wanakumbukumbu ya kutolewa na Chelsea kwenye michuano ya FA Februari 21 kwa kupata kipigo cha magoli 5-1.

Tangu mwaka 2010 timu hizo zimekutana mara 18 katika michuano mbali mbali huku City ikishinda mara 10 na Chelsea ikishinda tano wakienda sare mara tatu.

City imefikisha alama 60 ambao ni 12 nyuma ya vinara Leicester City wenye 72.

Post a Comment

 
Top