BOIPLUS SPORTS BLOG

 KLABU ya Chelsea imethibitisha kumsaini Kocha  Antonio Conte kuwa Meneja wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kocha huyo anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Italia 'Azzuri' atajiunga na klabu hiyo baada ya michuano ya Euro itakayofanyika nchini Ufaransa mwezi Juni.

Conte mwenye miaka 46 amesema "Nimejisiki vizuri kuchaguliwa kuwa meneja mpya wa Chelsea na pia kuwa kocha wa timu ya taifa langu hadi hapa tulipofika".

"Chelsea na soka la Uingereza linatazamwa duniani kote na mashabiki wana hisia kali ya mafanikio na ushindi uwanjani kama ilivyokuwa nchini Italia.

Conte anachukua nafasi iliyoachwa wazi  Jose Mourinho ambaye alitupiwa virago mwezi Disemba baada ya kuboronga mwanzoni mwa msimu huu.

Guus Hiddink ambaye amechaguliwa kuwa kocha wa muda tangu kutimuliwa kwa  Mourinho ameshasema atastaafu baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Conte anakuwa kocha wa tano raia wa Italia   kuifundisha Chelsea baada ya   Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na  Roberto Di Matteo.

Post a Comment

 
Top