BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
MSHAMBULIAJI tegemeo wa klabu ya Ndanda FC Atupele Green amekisifia kikosi cha Azam na kusema ni kizuri hasa wachezaji wake wa kimataifa huku akikiri kuwa wana mchango mkubwa sana kwa timu hiyo.

Mshambuliaji huyo aliyeisaidia timu yake kupata sare ya mabao 2-2 dhidi wanalambalamba amesema ukiwaangalia Azam mchezaji mmoja mmoja utagundua kuwa wako vizuri ila wao walicheza kama timu bila kuogopa kucheza ugenini na kupambana na wachezaji wenye majina makubwa.

"Umemuona Kipre (Tchetche) anavyocheza kwa kujituma na yule ndugu yake Balou na hata Pascal Wawa, wanacheza wakionekana kuwa ni mapro wa ukweli," amesema Atupele.

Kwa upande wake beki wa kushoto wa timu hiyo Paul Ngalema amesema kila mechi watakayocheza itakuwa ni fainali na wachezaji watapigana kufa na kupona kuhakikisha wanabaki ligi kuu.

Ndanda wanarejea Mtwara kwa ajili ya kuwapokea Mwadui kwa ajili ya mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Jumamosi Aprili 9.

Post a Comment

 
Top