BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
UKIWATAJA wachezaji ambao wapo mtegoni ndani ya kikosi cha Simba basi ni beki Mohamed Fhaki. Tangu asajiliwe hajawahi kucheza mechi yoyote ya mashindano hasa Ligi Kuu Bara ambayo timu hiyo inashiriki.

Fhaki alisajiliwa Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea JKT Ruvu ambapo ana mkataba wa mwaka mmoja mbele wa kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Karikakoo jijini Dar es Salaam.

Akiwa JKT Ruvu wakati huo inafundishwa na kocha Felix Minziro alikuwa hakosi kwenye kikosi cha kwanza cha maafande hao lakini mambo yamekuwa tofauti alipotua Simba kwani anakuwa mtazamaji timu yake inapocheza yeye anakuwa jukwaani.

Ni jambo gumu hasa katika kulinda kiwango chake lakini yeye anaamini kwamba ipo siku atapata nafasi ya kucheza kwani anajifua ipasavyo ili kuhakikisha kiwango chake hakishuki.

Fakhi ameiambia BOIPLUS: "Kiwango changu nakilinda kwa kufanya mazoezi vizuri, kupumzika vizuri tena kwa wakati muafaka na kula vizuri pia nakilinda kwa kuweza kufanya mazoezi yang binafsi na kutojihusisha na starehe ambazo zinaweza kunipotezea lengo langu na kiwango changu,".

Kwa sasa Fhaki si chaguo la kocha Jackson Mayanja ambaye hupendelea kuwatumia Juuko Murshid, Nova Lufunga ama Hassan Isihaka katika nafasi hiyo ila hali hiyo bado haijamkatisha tamaa beki hiyo.

"Ni kweli nilikuwa majeruhi lakini nilipona hivyo nasubiri kocha anipe nafasi, najituma mazoezini kama kawaida kwani lengo langu ni kucheza," alisema Fhaki

Post a Comment

 
Top