BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu
NAHODHA wa Azam John Bocco 'Adebayor' amekiri kutokuwa kwenye ubora wake katika mechi yao ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika  dhidi ya Esparance ndiyo maana alipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Katika mechi hiyo, Bocco alipoteza nafasi tatu za wazi wakati wapinzani wao wakiongoza bao moja huku akionekana kuwa mzito na kushindwa kuendana na kasi ya mchezo licha ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1. Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

"Sikuwa vizuri katika mchezo wetu huo na hii inawatokea wachezaji wengi mpira unaweza ukakukataa na siku nyingine inakuwa poa tu,"  alisema Bocco

Akizungumzia mechi yao ya marudiano itakayokwenda kuchezwa Tunisia Aprili 20, straika huyo alisema hiyo ni mechi ngumu kwao  kutokana na wapinzani wao  kupoteza mchezo wa kwanza ila timu yao  imejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi au sare ili wasonge mbele.

Bocco aliwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuwaombea ili wakafanye vizuri kwenye mchezo huo  wa marudiano.

Post a Comment

 
Top