BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
KUSHINDWA kuthamini wachezaji katika timu za Tanzania ndiyo sababu ya nyota wengi kutodumu katika timu na kuonekana kuwa wana matatizo jambo ambalo linachangia pia kushuka kwa viwango vyao.

Kauli hiyo imetolewa na winga wa Stand United ya Shinyanga, Haruna Chanongo ambaye ameingia kwenye mgogoro na kocha wake Patrick Liewig ambaye sasa mara kadhaa amekuwa akimpiga benchi.

Mapema mwaka huu Chanongo na Abuu Ubwa walienda kufanya majaribio katika timu ya TP Mazembe ya DR Congo baada ya kurejea ndipo alipojiingiza kwenye mgogoro na Liewig ambaye alidai kutowahitaji kwenye kikosi chake kwani walifanya utovu wa nidhamu kuondoka bila kuaga.

"Nimebakiza miezi miwili katika mkataba wangu nasubiri uishe tuachane kistaarabu siwezi kuendelea nao, nitakwenda sehemu nyingine kupata changamoto mpya.

 "Mawasiliano yote kutoka TP Mazembe yako kwa viongozi wangu lakini sipewi maendeleo yoyote toka kule ila mimi namuachia Mungu,'' alisema Chanongo ingawa hakutaka kuweka wazi ni timu gani atamwaga wino.

Chanongo alisajiliwa Stand United akitokea Simba ambao waliachana naye baada ya kuingia kwenye mgogoro na viongozi wake.

Post a Comment

 
Top