BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
LICHA ya kuwa katika nafasi mbaya ya kushuka daraja msimu huu lakini Coastal Union wametamba kumaliza kazi kwa Yanga hapo kesho kwenye mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la FA itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga

Mbali na hilo, Wagosi wa Kaya wamesema wanaendelea kupambana ili kujinusuru kushuka daraja msimu ujao japokuwa wana mechi tatu mkononi na wanashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22.

Akizungumza na BOIPLUS, beki wa timu hiyo Miraji Adam alisema: "Yanga ni timu kubwa tunaiheshimu ila na sisi tumejipanga kuhakikisha tunawafunga kwa kuwa ndiyo sehemu pekee kwenye matumaini,''

Mbali na kuyumba kwa timu hiyo, Miraji alisema kuwa hawajakata tamaa kwenye mbio za kujinasua kushuka daraja kitu pekee ambacho kitawasaidia ni kuongeza juhudi.

"Chelsea ndiyo mabingwa Uingereza msimu uliopita lakini kwa sasa wapo nafasi ya kumi baada ya kupitia katika hali kama yetu, hayo mambo yanatokea katika mpira, "alisema Miraji

Post a Comment

 
Top