BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Edward Christopher ambaye kwasasa anaichezea Toto Africans  ya Mwanza yupo tayari kurejea Simba endapo tu watampa donge nono.

Edo anayemalizia mkataba na Toto mwishoni mwa msimu huu alisema kuwa hawezi kuchagua timu ya kuichezea kwani hiyo ni ajira yake hivyo yupo tayari kufanyakazi na timu yoyote.

"Simba ni timu kubwa ina mashabiki wengi na pia wanalipa vizuri kulinganisha na Toto, wakinihitaji nipo tayari na sio wao tu hata Yanga na Azam wakiwa tayari nawatumikia, ukiwa mchezaji hupaswi kuchagua wapi ukacheze ila unatakiwa kuangalia masilahi yenyewe, " alisema Edo.

Edo alisema kuwa endapo Tanzania ingekuwa na mameneja wazuri wanaowaongoza wachezaji vijana basi nchi hii ingekuwa na timu bora ya Taifa kutoka mataifa mbalimbali ambayo wachezaji wangekwenda kucheza soka la kulipwa.

"Faridi Musa ameenda kufanya majaribio Hispania kwasababu ana watu wanaomsimamia, tumeona pia kwa kina Mbwana Samata na Thomas  Ulimwengu na wengineo waliofanikiwa kulikuwa na watu nyuma yao sisi tunawakosa ndiyo maana tupo hapa,'' alisema Edo.

Post a Comment

 
Top