BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
KIUNGO mkongwe wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph ameziambia Yanga na Azam FC kuwa kama watacheza kwa kujiamini na kujituma basi watashinda mechi zao za kimataifa za marudiano.

Kiungo huyo aliyewahi kuichezea Simba kabla ya kwenda kucheza nchini Norway alisema wachezaji wa timu hizo pia wazingatie nidhamu pamoja na kushambulia kwa tahadhari kubwa.

Yanga wamekwenda nchini Misri ambako watacheza na Al Ahly ambapo mechi ya awali iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 wakati Azam wao wapo Tunisia watacheza na Esperance, mechi ya awali Azam ilishinda bao 2-1.

"Timu zote zina nafasi ya kushinda ugenini kikubwa ni wachezaji kucheza kwa kushambulia kwa tahadhari na kutoruhusu goli la mapema ambalo litawatoa mchezoni  wachezaji wetu

"Kucheza na timu ya Al-Ahly au Esperance nyumbani kwao inabidi pia ujipange kucheza pungufu kwa kuwa wanapenda kuwashawishi waamuzi kutoa kadi hata mahala pasipo stahili," alisema Henry ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa Taifa Stars

Post a Comment

 
Top