BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
VIUNGO wa Azam Fc Himid Mao na Farid Mussa wanatarajia kukwea pipa kuelekea nchini Ubelgiji kufanya majaribio ya kusakata soka la kulipwa katika nchi hiyo ambayo inashika nafasi ya pili kwenye viwango ubora wa soka duniani.

Akizungumza na BOIPLUS msemaji wa Azam, Jaffar Idd alisema viungo hao watalazimika kukwea pipa mara baada ya mchezo wao dhidi ya Mtibwa utakaopigwa siku ya jumatano katika dimba la Manungu, Morogoro.

"Himid na Farid wataondoka kwenda Ubelgiji kufanya majaribio kwenye timu ambayo tutaitaja baadaye. Itakuwa ni baada ya mechi yetu na Mtibwa na kwamba watalazimika kuikosa mechi ya marudiano dhidi ya Esperance," alisema Jaffar.

Kama watafanikiwa kufuzu, nyota hao wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wataungana na mtanzania mwingine Mbwana Samatta anayekipiga kwenye klabu ya ligi kuu nchini humo, KRC Genk.

BOIPLUS inawatakia kila la heri Himid na Farid katika majaribio yao


Post a Comment

 
Top