BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
NUSU fainali ya kombe la FA itakayozikutanisha timu za Mwadui FC dhidi ya Azam na Coastal Union itakayopambana  na Yanga, itafanyika jumapili Aprili 24 huku kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' akijinasibu kuiondosha Azam.

Akizungumza na BOIPLUS Julio amefunguka kuwa atatumia mapungufu ya timu hiyo aliyoyaona katika mchezo wao dhidi ya Esparance na yatampatia ushindi katika uwanja Mwadui Complex siku ya Jumapili.

"Tunajua watakuja kwa  kasi baada ya kutolewa kombe la shirikisho lakini sisi tumeshajua udhaifu wao, tumejipanga na nia yetu ni kuchukua ubingwa huu ili mwakani tuiwakilishi nchi kimataifa," alisema Julio.

Wakati huo huo kocha wa timu ya Coastal Union Ally Jangalu alisema wameiweka timu kambini kwa ajili ya maadalizi ya nusu fainali hiyo dhidi ya Yanga hivyo ana uhakika mkubwa wa kupata ushindi hasa kwavile watakuwa nyumbani.

"Kama tuliweza kuwatoa Simba tukiwa ugenini kwa nini tushindwe kwa Yanga tukiwa nyumbani?," alihoji Jangalu.

Coastal walifika hatua hiyo baada ya kuitoa Simba kwa kuifunga magoli 2-1 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam huku wakiwa katika hatihati ya kushuka daraja kwenye ligi kuu inayoendelea.

Post a Comment

 
Top