BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
WAANDISHI wa habari za michezo wametakiwa kuripoti matukio ya mechi zote zinazoendelea katika ligi na sio kuangalia timu tatu tu zinazopigania ubingwa.

Kauli hiyo imetolewa na kocha wa timu ya Majimaji 'Wanalizombe',  Kali Ongala alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Azam ambao walilala kwa magoli 2-0 katika uwanja wa Chamazi Complex.

Ongala alisema kukosekana kwa usawa wa kuripotiwa kwa baadhi ya timu kunawaaminisha watanzania kuwa kuna timu tatu pekee ambazo  zinatoka jijini Dar es Salaam huku nyingine zikiwa zinasindikiza tu.

"Kabla ya mechi ya leo Majimaji tulicheza michezo saba ya ligi bila kupoteza nyumbani na ugenini, hakuna hata chombo kimoja kiliripoti habari hiyo lakini wangekuwa hao watatu wa juu vyombo vyote Radio TV na magazeti vingetangaza," alisema Kali.

Akizungumzia kuhusu timu zilizokuwa katika nafasi ya kutoshuka daraja na kuchukua ubingwa kupanga matokeo kutokana na na kujihakikishia kubaki ligi kuu Ongala alisema yeye hawezi kulizungumzia na wao kama Maji maji hawawezi kufanya hivyo.

"Kama mlivyoona tulipambana sana tukashindwa kutumia nafasi tulizopata wenzetu wamepata mbili wametumia, sisi hatuwezi kuruhusu kupoteza mchezo kisa tupo mahali salama kwenye ligi," alisema Kali.

Kwa vipindi tofauti kocha huyo aliwahi kutumikia timu za Yanga na Azam kabla ya kwenda nchini Uingereza kusomea fani ya ukocha.

Post a Comment

 
Top