BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
KIKAO cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kinatarajiwa kufanyika Jumapili, Mei Mosi jijini Dar es salaam huku wachezaji wanne wa Azam pamoja na kocha wao watawekwa kikaangoni kwa makosa mbalimbali.

Yanga ndiyo inafuatia kuwa na wachezaji wawili wote mastraika, Amissi Tambwe na Donald Ngoma wakati Simba wao mambo safi.

Kamati hiyo ya Nidhamu itapitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa.  Wafuatao kesi zao sitasikilizwa katika kikao hicho:

(i)  John Bocco – Azam FC

(ii) Shomari Kapombe – Azam FC

(iii) Aishi Manula – Azam FC

(iv) Amissi Tambwe – Yanga SC

(v) Donald Ngoma  - Yanga SC

(vi) Paulo Jinga – JKT Rwamkoma FC

(vii) Kipre Tchetche – Azam FC

(viii) Abel Katunda – Transit Camp

(ix) Zephlyn Laurian – JKT Rwamkoma FC

(x) Idrisa Mohamed – JKT Rwamkoma

(xi) DR. Mganaga Kitambi (Daktari) – Coastal Union

(xii)  Herry Chibakasa – Friends Rangers

(xiii) Ismail Nkulo – Polisi Dodoma

(xiv) Said Juma – Polisi Dodoma

(xv)  Idd Selaman – Polisi Dodoma

(xvi) Edward Amos – Polisi Dodoma

(xvii) Stewart Hall (Kocha)– Azam FC

Post a Comment

 
Top