BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar

BEKI wa Azam FC, Shomary Kapombe ameondoka leo kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake hivyo ataikosa mechi yao ya kimataifa dhidi ya Esperance ya Tunisia itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Azam wameamua kumpeleka kiraka huyo baada ya kuhisi kwamba huenda atakuwa na tatizo kwani afya yake haiko fiti tangu alipocheza mchezo wa kombe la FA dhidi ya Prisons.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd amethibitisha hilo "Ni kawaida kwetu sisi kama Azam kuwafanyia uchunguzi wa afya wachezaji wetu pale ambapo tunaona afya zao si nzuri.

"Hatufahamu tatizo hasa ni nini hivyo baada ya uchunguzi tutajua anasumbuliwa na kitu gani ila mchezo ujao tutamkosa kwani kesho (Ijumaa) ndio anaonana na daktari," alisema Jaffar

Kapombe alikosa mechi ya jana dhidi ya Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambapo Azam ilitoka sare ya mabao 2-2 pamoja na ile dhidi ya Toto African ya Mwanza waliyoambulia sare ya bao 1-1.

Post a Comment

 
Top