BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
KLABU ya KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta imezidi kuwa sumu kwa vigogo wa ligi kuu nchini Ubelgiji baada ya leo kuwatandika vinara wa ligi hiyo Club Brugge mabao 4-0.

Genk iliyofanikiwa kuingia hatua ya sita bora ya ligi hiyo (Play Off I) ilijipatia bao lake la kwanza katika dakika ya 14 kupitia kwa kiungo wake Onyinye Ndidi kabla Alejandro Pozuelo hajapachika la pili.

Dakika ya 45, mlinzi wa Brugge Thomas Meunier alijifunga bao akiwa katika harakati za kuokoa hivyo kuwapeleka Genk mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Genk waliendelea kuliandama lango la Brugge na dakika ya 73 walifanikiwa kupata bao la nne lililofungwa na Kere Uronen.

Dakika za mwisho mwisho Brugge walihamishia kambi yao langoni mwa Genk na kufanikiwa kupata mabao mawili ya haraka haraka yaliyofungwa na Ruud Vomer na Meurnier katika dakika za 80 na 84.

Samatta ambaye leo hakubahatika kupata bao, alitolewa katika dakika ya 76 nafasi yake ikichukuliwa na straika Nikos Karelis.

Kwa matokeo hayo Genk imefikisha pointi 33 ikiwa katika nafasi ya nne chini ya Brugge wanaoongoza (38), Anderletch(37) na Gent (34).

Post a Comment

 
Top