BOIPLUS SPORTS BLOG

HISPANIA
KIVUMBI cha ligi kuu nchini Hispania 'La liga' kimefikia patamu baada ya mbio za ubingwa kuendelea kuwa wazi kufuatia miamba mitatu inayopigania ufalme kushinda mechi zake.

Katika uwanja wa Estadio Municipal de Riazor mabingwa watetezi Barcelona walipata ushindi wa magoli 8-0 dhidi ya Deportivo la Coruna na kuendelea kujikitiza kileleni huku akifukuziwa kwa karibu na watoto wa jiji la Madrid, Atletico Madrid.

Luis Suarez alifunga magoli manne peke yake huku Lionel Messi,Ivan Rakitic, Marc Batra na Neymar wakifunga goli moja moja.

Mchezo mwingine ulikuwa katika uwanja wa San Names Barria ambapo Atletico  walipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji Athletic Club Bilbao huku bao pekee likiwekwa kimiani na Fernando Torres.


Santiago Bernabeu wenyeji Real Madrid waliwachapa manyambizi wa manjano Villarreal magoli 3-0 na kubakisha alama moja pekee kuwafikia vinara Barcelona.

Magoli ya Real yaliwekwa kimiani na Karim Benzema, Luca Modric na Lucas Vesquez.

Msimamo wa la liga unaonesha Barcelona wanaongoza wakiwa na alama 79 sawa na Atletico Madrid tofauti ya magoli ya kufunga na Madrid inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 78 huku timu zote zikishuka dimbani mara  34.

Post a Comment

 
Top