BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MABINGWA mara kumi wa klabu bingwa barani ulaya Real Madrid imelazimishwa sare ya kutofungana dhidi ya Manchester city katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali kwenye uwanja wa Etihad jijini Manchester.

Real iliingia uwanjani bila mchezaji bora wa dunia mara tatu Cristiano Ronaldo ambaye anasumbuliwa na majeruhi na kuwafanya mabingwa hao kukosa ubunifu wanapokuwa katika eneo la mwisho la wenyeji.

City walionekana kuwadhibiti Real ambapo katika eneo la kiungo wabrazil Fernando na Fernandinho waliweza kutuliza mashambulizi na kumiliki mpira kwa asilimia kubwa zaidi ya wageni.

Hata hivyo juhudi za golikipa Joe Hart ziliisaidia City kuepuka kipigo baada ya kuokoa mara kadhaa mashambulizi ya Gareth Bale na beki   Pepe.

Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Santiago Bernabeu nchini Hispania.

Man City :Joe Hart,Sagna,Clichy,Otamendi,Kompany,Fernandinho,Navas,Fernando, Aguero,Silva,De Bruyne.

Real:Navas,Carvajal,Marcelo,Pepe,Ramos,Casemiro,Kroos,Modric,Benzema,Valquez,Bale.

Post a Comment

 
Top