BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
TIMU ya Majimaji 'Wanalizombe' ya mjini Songea wamenogewa na huduma ya straika wao Danny Mrwanda ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu, unajua wamesemaje?...."Hatoki mtu hapa."

Katibu mkuu wa Majimaji John Mbano ameifungukia BOIPLUS kuwa mchango mkubwa wa nahodha huyo katika kikosi chao ndio unaowafanya wasifikirie kuachananae mara mkataba wake utakapomalizika.

"Mkataba na Mrwanda unamalizika mwishoni mwaka msimu na hatutarajii kumuacha kumuacha mchezaji muhimu kama huyu, nina imani tutakuwa nae msimu ujao.

"Tutafanyanae mazungumzo ya kumuongezea mkataba mara baada ya ligi kwisha, bila shaka tutaelewana tu ili aendelee kuwepo hapa," alisema Mbano.

Tayari mshambuliaji huyo ameshafunga magoli sita kwenye ligi na kuisaidia timu hiyo kukamata nafasi ya tisa baada ya kukusanya alama 33.

Licha ya Mrwanda aliyewahi kuzitumikia timu za Simba na Yanga katika nyakati tofauti kabla hajatimkia ughaibuni, Majimaji pia inajivunia huduma ya mkongwe mwingine Godfrey Taita.

Post a Comment

 
Top