BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma

MAJOGOO wa jiji la London klabu ya Liverpool imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Europa baada ya kuifunga  Borussia Dortmund magoli 4-3 kwenye uwanja wa Anfield .

Dortmund walitumia dakika tisa kupata magoli mawili kupitia Henrick Mikhtarian aliyefunga dakika ya tano na Pierre Emerick Aubemeyang dakika ya tisa magoli yaliyodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili Divock Origi aliipatia Liverpool goli la kwanza dakika ya 48 kabla Marco Reus hajafunga goli la tatu dakika ya 53. Philipe Coutinho aliifungia Liverpool dakika ya 66 huku Mamadou Sakho akisawazisha katika dakika ya  78 na Dejan Lovren kufunga bao la ushindi dakika ya 90.

Liverpool imeitoa Dortmund kwa jumla ya magoli 5-4 baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 katika dimba la Signal Iduna Park Ujerumani.

Timu nyingine zilizofuzu ni Sevilla iliyoitoa Athletic Club Bilbao kwa penati 5-4 baada ya sare ya 3-3. Shakhtah Donesk imeitoa Braga kwa kuifunga magoli 4-0 na Villarreal imeifurumusha Sparta Prague kwa magoli 4-2

Droo ya michuano hii itapangwa baada ya ile ya klabu bingwa barani Ulaya jijini Zurich mchana wa Leo.

Post a Comment

 
Top