BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) juzi Jumatano iliyakamata magari matano ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) tukio ambalo limewavuruga viongozi wa shirikisho hilo ambapo jana jioni Rais Jamal Malinzi aliamua kumwaga manyanga.

Malinzi alifikia hatua hiyo baada ya kuona TRA inazidi kuwarudisha nyuma katika mipango yao ya maendeleo kwani hata mwaka jana walifunga akaunti zote za TFF kwa kudai Sh 1.6 bilioni deni ambalo  linawatesa TFF mpaka sasa.

TRA inaidai TFF Sh 1.1 bilioni kwani katika deni lao TFF walifanikiwa kulipa Sh 400 milioni pekee kati ya hizo huku kwenye akaunti zao zilizozuiliwa na TRA zikiwa na zaidi ya Sh 150 milioni fedha ambayo haikuweza kumaliza deni hilo.

Fedha hizo ni deni la kodi ya ongezeko la thamani (VAT), makato ya kodi ya lipa upatavyo (PAYE) kwa mishahara ya wafanyakazi wa TFF na wachezaji wa kigeni pamoja na kodi ya makocha wanne wa kigeni akiwemo Marcio Maximo, Jan Poulsen na Kim Poulsen na mapato ya mechi kati ya Brazil na Taifa Stars iliyochezwa mwaka 2014.

TFF sasa inahaha jinsi gani ya kwenda kukomboa magari yao ambayo yapo kwenye maegesho ya kuuzia magari ya Yono Action Mart huku sharti kubwa walilopewa ni kulipa fedha hizo kama watakavyokubaliana.


Leo ni Aprili mosi, siku ya wajinga duniani, hivyo kujiuzulu kwa Malinzi si taarifa ya kweli ila kukamatwa kwa magari ya TFF ni kweli.

Post a Comment

 
Top