BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER United imetinga fainali ya kombe la FA baada ya kuipiga Everton magoli 2-1 katika uwanja wa Wembley.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku mashetani wekundu wakitawala zaidi sehemu ya kati ya uwanja na Toffee wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini umahiri wa David De Gea uliisaidia United.

Dakika ya 34 Marouane Fellain aliipatia goli la kwanza United baada ya kupiga 'gonga' na Anthon Martial kupiga krosi safi iliyokumkuta mfungaji.

Mpaka wanakwenda mapumziko mashetani wekundu walikuwa mbele kwa goli moja.


Kipindi cha pili mpira uliendelea kuwa wa kasi huku Everton wakifanya mashambulizi ya kushtukiza na dakika 56 beki Fosu- Mensah alimchezea rafu kiungo Ross Barkley kwenye eneo la hatari na mwamuzi aliamuru ipigwe penati na mkwaju huo wa Romelu Lukaku ulipanguliwa na golikipa David De Gea.

Dakika 75 beki Chris Smalling alijifunga katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Jofrey Delfoue

Ikiwa imebaki dakika moja kumalizika kwa mchezo huo Martial iliipatia United goli la ushindi baada ya kupokea pasi toka kwa kiungo Ander Herrera.

United inasubiri mshindi kati ya Watford na Crystal Palace utakaopigwa kesho katika uwanja huo huo wa Wembley.

Post a Comment

 
Top